Sera ya Faragha

                

Tarehe ya Kuanza Kutumika: [22/04/2026]

Kwenye Nyansaho Foundation, tumejizatiti kulinda faragha ya wafadhili wetu, wanufaika, wanao jitolea, washirika, na wageni wa tovuti yetu. Sera hii ya Faragha inaelezea jinsi tunavyokusanya, kutumia, na kulinda taarifa zako unapotumia tovuti yetu au njia nyingine za mawasiliano.

1. Taarifa Tunazokusanya

Tunaweza kukusanya aina zifuatazo za taarifa:

Taarifa Binafsi: Jina, anuani ya barua pepe, anuani ya makazi, namba ya simu, Vyeti au Wasifu wako kielimu na kikazi (CV), Wasifu wa taasisi au faili za taasisi unazotutumia kupitia fomu, na taarifa za malipo (ikiwa utatoa mchango). Taarifa hizi zinakusanywa kwa hiari yako, na zinatumika kwa kwaajili ya kuwasiliana nawe au kukupa huduma husika uliyo omba. Taarifa za Hiari: Taarifa unazotoa unapowasiliana nasi, kujisajili kwa huduma au kujaza fomu kwenye tovuti yetu.

2. Jinsi Tunavyotumia Taarifa Zako

Tunatumia taarifa zako kwa ajili ya:

Kuchakata michango na kutuma risiti. Kuwasiliana nawe kuhusu programu, huduma, matukio, na kampeni zetu. Kujibu maswali yako na kutoa msaada. Kudumisha kumbukumbu sahihi kwa ajili ya taarifa na kufuata sheria. Kuboresha tovuti, mawasiliano, na huduma zetu.

3. Kushiriki na Kufichua Taarifa

Hatuuzi, kubadilishana, au kukodisha taarifa zako binafsi. Tunaweza kushiriki taarifa tu katika hali zifuatazo:

Na watoa huduma waliotuamini wanaosaidia kuendesha tovuti yetu au kusimamia michango, chini ya makubaliano madhubuti ya faragha. Ikihitajika kwaajili ya kukupa huduma uliyoomba, kwa idhini yako. Mfano: Kutumia taarifa zako kukusajili kwaajili ya masomo uliyo hitaji, kukulipia ada, nakadhalika. Ikihitajika kisheria, kwa mfano kufuata wajibu wa kisheria au kulinda haki za Nyansaho Foundation.

4. Usalama wa Taarifa

Tunachukua hatua za kiufundi na kiutawala kulinda taarifa zako dhidi ya upatikanaji usioidhinishwa, ufichuaji, au matumizi mabaya. Hii ni pamoja na kutumia seva salama, zana za usimbaji, na kuzuia upatikanaji wa taarifa zako binafsi na kuruhusu upatikanaji wa taarifa zako binafsi kwa wafanyakazi walioidhinishwa pekee kushughulikia huduma uliyo hitaji kwetu.

5. Haki Zako

Una haki ya:

Kuomba kuona taarifa zako binafsi. Kurekebisha au kusasisha taarifa zako. Kuomba taarifa zako zifutwe (pale ambapo kisheria inaruhusu). Kujiondoa kwenye barua pepe au jarida letu.

Ili kutumia haki hizi, wasiliana nasi kupitia info@nyansahofoundation.or.tz.

6. Vihifadhi Taarifa/Vidakuzi (Cookie) na Takwimu za Tovuti

Tovuti yetu kwasasa haitumii teknolojia yoyote ya ukusanyaji wa taarifa zisizo binafsi kama (Ipaddress, Browser, OS, Eneo ulilopo, aina ya kifaa unachotumia) na wala haihifadhi vidakuzi (cookies) za aina zozote kwasasa. Endapo kutakuwepo ongezeko la matumizi yoyote yale ya ukusanyaji wa taarifa zisizo binafsi na matumizi ya vihifadhi taarifa/Vidakuzi (cookies) basi tutaweka fomu ya kuomba idhini ya matumizi ya teknolojia hizo kabla hazijatumika kwenye kifaa chako. Pamoja na kuwepo kwa uwazi katika sera ya faragha kuhusu teknolojia zipi zinatumika, zinafanya kazi zipi na taarifa zake zinatumika vipi.

7. Viungo vya Wavuti za Wengine

Tovuti yetu inaweza kuwa na viungo kwenda kwenye tovuti za watu wengine mfano: Facebook, Linkedin, na Instagram. Hatuwajibiki kwa sera za faragha au maudhui ya tovuti hizo.

8. Maboresho ya Sera Hii

Tunaweza kuboresha sera hii mara kwa mara. Mabadiliko yoyote yatawekwa kwenye ukurasa huu pamoja na tarehe mpya ya kuanza kutumika. Tunakuhimiza kutembelea ukurasa huu mara kwa mara.

9. Wasiliana Nasi

Ikiwa una maswali au wasiwasi kuhusu Sera hii ya Faragha, tafadhali wasiliana nasi:

Barua Pepe: info@nyansahofoundation.or.tz Anwani: Dar es Salaam, Tanzania Tovuti: https://nyansahofoundation.or.tz